← Rudi Nyumbani

Jinsi ya Kupokea Malipo ya WiFi kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa kwa Kutumia API

Unataka mteja alipe kwa simu yake na aunganishwe papo hapo, bila wewe kupokea pesa mkononi wala kuthibitisha muamala. Hilo linafanywa na API ya malipo. Makala hii inaeleza API ni nini, watoa huduma unaoweza kutumia, na hatua za kuiunganisha na WiFi yako.

API ya Malipo ni Nini?

API ni njia ya mifumo miwili kuzungumza yenyewe. Kwa biashara ya WiFi, mfumo wako wa billing unamwambia mtoa huduma wa malipo: mtoze mteja huyu kiasi hiki. Mtoa huduma anamtumia mteja ombi la kuweka PIN, kisha anarudisha jibu: amelipa au hajalipa. Hakuna binadamu katikati.

Bila API, unalazimika kusoma ujumbe wa muamala na kumfungulia mteja kwa mkono. Hiyo haiwezekani usiku, na haiwezekani wateja wakiwa wengi.

Kinachotokea Mteja Anapolipa

Pesa inaingia kwenye akaunti yako uliyoifungua kwa mtoa huduma wa malipo. Wewe ndiye mwenye akaunti hiyo.

Watoa Huduma wa Malipo Unaoweza Kuunganisha

UpesiLipa inaunganishwa na API za watoa huduma hawa wa Tanzania. Unachagua mmoja, unafungua akaunti kwake, kisha unabandika funguo zake (API keys) kwenye dashibodi yako:

Mtoa hudumaUnachobandika kwenye dashibodi
ClickPesaClient ID na API key
FimiPaySecret key, na Webhook secret
SnippeAPI key, na Webhook secret
SelcomVendor ID, API key na API Secret
AzamPayApp name, Client ID, Client Secret na Token key
SonicPesaAPI key, na API Secret (si lazima)
PalmPesaAPI key, na User ID kama dashibodi yao inaionesha
PlusPesaPublic Key na Secret Key, na Callback secret (si lazima)

Vigezo vya kufungua akaunti, ada za miamala na muda wa kupata pesa vinapangwa na mtoa huduma mwenyewe. Uliza kwao kabla ya kuchagua. Chaguo la mtoa huduma ni lako.

Hatua 5 za Kuunganisha

Makosa Yanayofanya Malipo Yashindikane

01

Funguo za majaribio

Umebandika funguo za sandbox badala ya live. Mteja haoni ombi lolote kwenye simu yake.

02

Akaunti haijathibitishwa

Mtoa huduma bado hajakamilisha uthibitisho wa biashara yako, kwa hiyo anakataa kila muamala.

03

Funguo imekatika

Herufi moja imekosekana wakati wa kunakili. Bandika upya ukihakikisha umenakili yote.

04

Webhook haijawekwa

Mteja amelipa, lakini jibu halifiki. Hakikisha anwani ya taarifa imewekwa upande wa mtoa huduma.

Kwenye dashibodi ya UpesiLipa kila malipo yaliyoshindikana yanaonekana pamoja na sababu yake, kwa hiyo hubahatishi tatizo liko wapi.

Linda Funguo Zako Kama Nenosiri

API key ni ufunguo wa akaunti yako ya malipo. Usiitume kwenye magrupu ya WhatsApp, usiipige picha, na usimpe mtu usiyemwamini. Ukihisi imevuja, itengeneze upya kwa mtoa huduma na ubandike mpya.

Na Mteja Asiye na Salio?

Si kila mteja ana pesa kwenye simu. Ndiyo maana malipo ya simu yanakwenda pamoja na vocha: mteja analipa pesa taslimu, anapewa kodi, anaiingiza kwenye ukurasa ule ule. Njia zote mbili zinafanya kazi kwa wakati mmoja.

Unganisha Malipo ya Simu Leo

Jisajili bure, chagua mtoa huduma wako wa malipo, bandika funguo, na ujaribu kwa simu yako. Ukikwama kwenye hatua yoyote, tuko WhatsApp.

Jisajili Bure

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

API ya malipo ni nini?

Ni njia ya mfumo wa billing kuzungumza na mtoa huduma wa malipo. Mfumo unaomba mteja atozwe, mtoa huduma anamtumia mteja ombi la PIN, kisha anarudisha jibu kama amelipa au la.

Naweza kupokea malipo ya WiFi kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa?

Ndiyo. Mtoa huduma wa malipo unayemuunganisha ndiye anayekupa mitandao hiyo. Mteja anaandika namba yake na anapokea ombi la malipo kwenye simu.

UpesiLipa inaunganishwa na watoa huduma gani wa malipo?

ClickPesa, FimiPay, Snippe, Selcom, AzamPay, SonicPesa, PalmPesa na PlusPesa. Unachagua mmoja na kubandika funguo zake kwenye dashibodi.

Pesa za wateja zinaingia wapi?

Zinaingia kwenye akaunti yako uliyoifungua kwa mtoa huduma wa malipo uliyemchagua.

Ada za miamala ni kiasi gani?

Kila mtoa huduma ana ada zake. Uliza kwao kabla ya kuchagua, kwa sababu ada na muda wa kupata pesa vinatofautiana.

Kwa nini mteja haoni ombi la malipo kwenye simu?

Sababu za kawaida ni funguo za majaribio badala ya live, akaunti ya malipo isiyothibitishwa, au funguo iliyonakiliwa nusu. Dashibodi inakuonesha sababu ya kila malipo yaliyoshindikana.

Soma Pia

How to accept WiFi payments by M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money and HaloPesa through a payment API in Tanzania. UpesiLipa connects to ClickPesa, FimiPay, Snippe, Selcom, AzamPay, SonicPesa, PalmPesa and PlusPesa: open an account with one, paste its API keys, test with your own phone.